Kama ungekuwa Myahudi mwaminifu mwaka wa AD 27, ungekua umeamini nini? Ungekuwa unamwamini nani? Ungeweka uaminifu wako wapi?
Maisha yako yote, ungekuwaumefundishwa na wazazi wako, walimu, na makuhani kwamba wewe uu sehemu ya watu maalum waliochaguliwa na Mungu, watu walio na maandiko yaliyovuviwa na manabii na walio kuwa wakingoja ujio wa Masihi.
Maisha yako yote, ulifundishwa kwamba dini zote zingine duniani zilikuwa za uongo.
Maisha yako yote, umekuwa ukishiriki Sabato kila wiki, kutoa dhabihu hekaluni mara kwa mara, na kusherehekea sikukuu za kila mwaka kama vile Pasaka na Siku ya Upatanisho (Yom Kippur).
Maisha yako yote, umekuwa ukiwaamini viongozi wa dini—makuhani, baraza la Sanhedrin—kufafanua maandiko matakatifu, kukuambia wajibu wako kwa Mungu, kueleza kilicho sahihi au kibaya kwa dini, na kubaini uzushi na kukufuru.
Na maisha yako yote yangekuwa mzigo—maisha chini ya hofu ya dhambi, uzito wa masharti ya dini, hofu ya kushindwa, shaka isiyokoma, hisia ya kutofaa, wasiwasi wa kudumu kwamba labda licha ya kulipa zaka zako zote, kutoa dhabihu zote, na jitihada zako zote za kufuata kanuni, bado hukukubalika na Mungu.
Kama ungekuwa Myahudi huyo, ungefanya nini? Je, kulikuwa na taasisi nyingine ya kidini ambayo Mungu alikuwa akiitumia zaidi ya Israeli? Kulikuwa na Biblia bora zaidi yenye ufunuo sahihi zaidi kuliko Torati?
Je, hilo lingemaanisha kwamba uongozi wa taasisi ya Kiyahudi ulikuwa unafundisha ukweli?
Ikiwa ungekuwa Myahudi miaka 2000 iliyopita, ingekuwa busara kuwatumainia makuhani, Walawi na Sanhedrini kuamua ni nini kilicho kweli? Nini mapenzi ya Mungu? Dhambi ni nini? Mtu anaokokaje kutoka katika dhambi?
Viongozi wa dini wa Kiyahudi walikosea wapi? Walifunika tafsiri zao za Maandiko kwa ufahamu usio sahihi wa sheria. Waliona sheria ya Mungu ikifanya kazi kama sheria za kibinadamu—kanuni zilizowekwa ambazo zinahitaji adhabu za kubuni. Kwa hivyo walipotosha ibada na mifano kuwa masharti ya moja kwa moja ya wokovu, badala ya maonyesho, mfano na somo la kivitendo lililokusudiwa kufundisha ukweli.
Kisha Yesu akaja na akafundisha kwa mamlaka—mamlaka ya jinsi uhalisia unavyofanya kazi. Hadithi Zake zote ziliwafundisha watu kwamba sheria za Mungu ni sheria za mpangilio wa uumbaji—kanuni za jinsi maisha yanavyofanya kazi. Yesu alivunja sheria za dini zilizowekwa na wanadamu ili kuendeleza ufalme wa mbinguni. Yesu aliponya siku ya Sabato na kula na makahaba, watoza ushuru, na Wasamaria. Kwa nini?
Kwa sababu Yesu hushughulika na uhalisia—na uhalisia ni kwamba Mungu aliumba wanadamu kama jamii moja Edeni.
Adamu alijipata katika hali ya dhambi, hivyo kila mwanadamu huzaliwa katika hali hiyo ya dhambi (Zaburi 51:5); kila mtu anahitaji tiba ile ile ya shida hii; na Yesu alikuja kuondoa dhambi ya ulimwengu (Yohana 1:29) ili kutoa tiba ya hali yetu ya dhambi, kuwaokoa na kuwaponya wote wanaoshiriki kile alichotoa (Wagalatia 2:20; 2 Petro 1:4).
Dhambi haiwezi kutatuliwa kwa sheria na kufuata sheria—bali kwa uumbaji upya, uponyaji, usafishaji wa moyo na akili kwa nguvu ya uumbaji wa Mungu!
Yesu alisema,
“Kwa maana Mungu aliupenda ulimwengu kiasi cha kumtoa Mwanae pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwanae kuuhukumu ulimwengu bali auokoe.” (Yohana 3:16,17).
“Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jifungeni nira yangu; jifunzeni kutoka kwangu; kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha nafsini mwenu. Kwa maana nira yangu ni rahisi, na mzigo wangu ni mwepesi.” ( Mathayo 11:28 -30
Na viongozi wa dini—viongozi wa watu wa Mungu walioteuliwa—walipomwona Yesu akiponya, kubariki, na kusamehe, walisema:
“Je, sisi hatusemi kwa haki ya kuwa wewe ni Msamaria na una pepo?” (Yohana 8:48).
Kama ungekuwa Myahudi mwaminifu miaka 2,000 iliyopita ukifanya kazi kwa ajili ya “kanisa,” ungejibuje? kama viongozi wako wangekuuliza maswali haya kama walivyouliza wafuasi wao:
Hatimaye wale walinzi wa Hekalu waliokuwa wametumwa kum kamata Yesu, walirudi kwa makuhani wakuu na Mafarisayo. Wakauli zwa, “Mbona hamkumleta ?”
Wale walinzi wakajibu, “Hakuna mtu ambaye amewahi kufundisha kama yeye.”
Mafarisayo wakajibu, “Ameweza kuwa danganya hata ninyi? Je, mmewahi kuona kiongozi ye yote au mmoja wa Mafarisayo ambaye amemwamini? Lakini huu umati wa watu wasiojua sheria ya Musa, wamelaaniwa.” (Yohana 7:45–49).
Kwa hiyo, kama ungekuwa Myahudi mwaminifu miaka 2,000 iliyopita, ungeendelea kuwa mwaminifu kwa kushikamana na dhehebu lako, mafundisho ya walimu, makuhani, Walawi, na Sanhedrin? Au kama ungelifuata viongozi hao wa mfumo wa Mungu uliobarikiwa, ungegeuka kutoka uaminifu kwenda uasi na kujiunga nao katika kumsulubisha Yesu?
Na leo je?
Kama wewe ni Mkristo mwaminifu, unayehusishwa na dhehebu linalodaiwa kuitwa na Mungu kupeleka injili kwa ulimwengu na kuendeleza mafundisho “sahihi,” je, utaweza kubaki mwaminifu kama ukiwaachia wachungaji, makasisi, maprofesa wa theolojia, na viongozi wa kanisa wafikirie badala yako—au sharti ufikirie mwenyewe na ujue ukweli mwenyewe?
Kama Paulo alivyoshauri katika Warumi 14:5, je, hautakiwi kushawishika kabisa katika akili yako kuhusu kilicho kweli? Inawezekana kwamba ili kubaki mwaminifu kwa Yesu, itakulazimu kuwa kama Petro, Paulo, na mitume wengine—na kukataa mafundisho ya viongozi wa kanisa lako?
Haya si mambo ya kubuni—ni historia. Yametokea tena na tena. Kama mwanzilishi mmoja wa Kanisa la Waadventista alivyoandika katika
Tumaini La Vizazi Vyote:
“Sanhedrini walikuwa wameukataa ujumbe wa Kristo na walikuwa wameazimia kumuua; kwa hiyo Yesu aliondoka Yerusalemu, kutoka kwa makuhani, hekalu, viongozi wa dini, watu waliokuwa wamefundishwa katika sheria, na akageukia kundi jingine ili kulitangazia ujumbe Wake, na kuwakusanya wale ambao wangeibeba injili kwa mataifa yote.
Kama vile nuru na uzima wa wanadamu vilivyokataliwa na viongozi wa kidini katika siku za Kristo, ndivyo vilivyokataliwa katika kila kizazi kilichofuata. Mara kwa mara historia ya Kristo kujitenga na Uyahudi imerudiwa. Wakati Wanamatengenezo walipohubiri neno la Mungu, hawakuwa na wazo la kujitenga na kanisa lililoanzishwa; lakini viongozi wa kidini hawakuvumilia nuru hiyo, na wale waliokuwa wakiibeba walilazimishwa kutafuta kundi jingine lililokuwa likitamani ukweli. Katika siku zetu wachache miongoni mwa wanaodai kuwa wafuasi wa Wanamatengenezo wanaongozwa na roho yao. Wachache wanasikiliza sauti ya Mungu na wako tayari kukubali ukweli katika sura yoyote utakayowasilishwa. Mara nyingi wale wanaofuata nyayo za Wanamatengenezo hulazimika kugeuka kutoka kwa makanisa wanayoyapenda ili watangaze mafundisho ya wazi ya neno la Mungu. Na mara nyingi wale wanaotafuta nuru hulazimishwa na mafundisho hayo hayo kuyaacha makanisa ya baba zao ili waweze kutii.
Ninakutia moyo: Usije ukaanguka katika mtego wa kusalimisha akili yako kwa wengine; daima fikiria mwenyewe na ubaki mwaminifu kwa Yesu kuliko mtu yeyote mwingine.












using your credit or debit card (no PayPal account needed, unless you want to set up a monthly, recurring payment).
instead?